Habari ilitufikia alfarjiri na mapema kuwa jirani yetu Veronica ametekwa nyara akiwa barabarani akielekea Ngosi mtaa wa kipusi. Habari zinasema kuwa alikuwa amevalia nguo za kijani kibichi na pia alipenda kuvaa kofia ya rangi ya theluji. Watu walikuwa wakisema kuwa urembo aliokuwa nao Veronica haukuweza kusemwa wala kuandikwa.
Mtaa wa Peleleza ambao Veronica alinyakuliwa huwa ni mtaa wa majambazi. Polisi walijaribu kurekebisha lakini hawakufua dafu kwa kuwa mmoja wao aliweza kuuliwa na wengine kukatwa masikio. Kwa hivyo ilikuwa hata mngeni kupita mtaa huo bila kupata tatizo ni bahati.
Wananchi wa mtaa wetu walipandwa na hasira waliposikia kitendo hicho cha Veronica. Mtaa wetu wa Mabomani uliweza uliweza kufanya mkutano wa dharura katika Boma la wekesa babake Veronica. Baada ya mkutano wa mjadala huo mrefu polisi waliwezwa kuitwa na kuelezewa kitendo hicho .
Polisi na wazee wa mtaa waliandama kwenda kutafuta Veronica wakiwa kwa hasira Sana. Watu walibaki kwa kikao wakisubiria matokeo Bora ya kumuona Veronica.
Hakuna mda mrefu polisi waliondkana wakifetua vitoa machozi na kukimbizana wakielekea undani wa kijiji hicho. Nao wananchi walionekana kwa mbali wakiwa na shangwe wakiimba nyimbo za furaha kuonyesha Veronica ameoneka. Bahati iliweje kwa Veronica kuonekana na wananchi kisha wakambeba juu juu kuonyesha ishara ya ushindi . Mzee Wekesa aliandalia wananchi chai na vitoeo wakasherekea pamoja .

Discover more from Lifestyle
Subscribe to get the latest posts sent to your email.
@readers there is only one way I can improve and that’s is through comment section.
LikeLike